Mhe. Mwanaidi amewataka wananchi wa Kata ya Kaniha Mkoani Kagera kuwa walinzi wa miundombinu inayojengwa.

Uongozi wa Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera umetakiwa kuweka mifumo madhubuti ya usimamizi wa miradi mbalimbali inayojengwa na Serikali kwa kuzingatia thamani halisi ya fedha inayotumika katika ujenzi wa miundombinu hiyo. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis katika ziara yake kwenye zahanati